Miners go on Strike
Chama cha wachimba migodio nchini Afrika Kusini kimesema kuwa wanachama wake katika wa madini ya platinum wameanza mgomo kuhusiana na malipo duni. Usimamizi wa kampuni ya northam platinum umetoa nyongeza ya asilimia nane ya mshahara , lakini wachimba migodi hao wanasisitiza kuwa lazima wapewe nyongeza ya asilimia 15. Chama hicho kinasema kuwa wafanyakazi elfu nane wa kampuni hiyo walio wanachama wake wameanza mgomo huo. Hata hivyo, msemaji wa chama chao alinukuliwa akisema kuwa haijabainika wazi, idadi kamili ya wafanyakazi wanaouunga mkono mgomo huo. Mgomo huo ni wa hivi punde kuikumba afrika kusini kuhusiana na malipo duni kwa wafanyakazi wake. Wafanyakazi wa umma wakiwemo wahudumu wa afya, polisi, waalimu na maafisa wa uhamiaji wamekuwa wakifanya mgomo wakitaka nyongeza ya asilimia nane nukta tano ya mshahara .serikali ya afrika kusini tayari imewapa nyongeza ya asilimia saba nukta tano.  
-------------
South Africa’s miners have gone on strike in the latest series of walk-outs in the country over pay. The miners are among millions of workers who have recently taken industrial action rejecting a revised pay deal which was due to end their three week strike.